Asalaam aleykum ndugu jamaa na marafiki karibuni katika Uwanja wa vijana, ambapo tutapata kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu vijana. Kuna usemi usemao kuwa vijana ni taifa la kesho ukimaanisha kuwa ulimwengu ujao utatawaliwa na vijana wa leo. Sisi kama vijana yatupasa kuelewa kuwa ni muhimu kwetu kuwa na malengo ambayo baadae yatatupeleka kwenye ndoto zetu au vile ambavyo tunatarajia kuvipata baadae. Vijana ndoto zetu zinayeyuka kutokana na mambo mbalimbali yanayoibuka kati yetu, kwa mfano chuki miongoni mwetu ambapo mtu mmoja anakuwa hapendi maendeleo ya mwenzake kwa namna moja au nyingine, kujiingiza kwenye makundi mabaya ambayo saa zote yanawaza mambo mabaya kutokana na uchu wa kutaka kutajilika kwa haraka. Hapo ndipo utakuta vijana wanajiingiza kwenye wizi, ujambazi, ukahaba na mambo mengine ambayo hayapendezi kwa jamii.
Napenda kuwaambia kuwa wote tumezaliwa sawa japokuwa kuna matajili na masikini, hakuna alieumbiwa shida maisha yake yote. Kama hujapata leo basi utapata kesho kwa hiyo usikate tamaa endelea kujituma kadri ya uwezo wako ipo siku mambo yatakuwa sawa.
No comments:
Post a Comment